Wednesday, December 17, 2014

On 8:22 AM by Unknown   No comments




Stori: Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
Mamaaa! Muuza nyago kwenye sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ ameibuka na kuanika kijasiri kuwa ‘ameshambonji’ na mastaa wa kiume 15 wa Bongo huku akisema kitendo hicho hakijamuondolea hadhi yake, Risasi Mchanganyiko linatiririsha.



Muuza nyago kwenye sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’.



Akizungumza katika mahojiano maalum na waandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar, Bozi alitamka hayo kwa kujiamini zaidi.Mahojiano kati ya msanii huyo na Risasi Mchanganyiko yalikuwa kama ifuatavyo:

Risasi: “Mzima Bozi?”
Bozi: “Mi mzima sana. Enhe! Karibuni  maana nasikia mmenitafuta sana, kuna nini?”
Risasi: “Tumeshakaribia. Sisi tunataka kufanya mahojiano na wewe kuhusu sanaa kwa ujumla, ugumu na wepesi wake.”
Bozi: “Oke, sawa.”


Fatuma Ayubu ‘Bozi’akipozi.
Risasi: “Oke, labda kwa kuanzia Bozi, umeshapambana na ugumu wowote kwenye fani? Kama vile kulazimishwa kuvaa nguo za hasara kutokana na ‘sini’ unayoigiza?”Bozi: “Bahati nzuri nguo tunazovaa kwenye ‘viwanja’ kujirusha ndizo hizohizo hata tunazovaa mtaani. Kwa hiyo hakuna ugumu wowote.”
Risasi: “Wasanii mnaoibukia siku hizi mnadaiwa mmevamia fani ili kuuza sura na kutafuta mabwana, hasa mapedeshee. Kuna ukweli?”Bozi: “Pengine wapo lakini mimi nimeingia kwenye fani kwa sababu ya msukumo wa kipaji changu na si kutafuta mabwana. Kama mabwana mbona wapo mastaa kibao nilishalala nao kabla.” 

0 comments:

Post a Comment