Friday, December 26, 2014
On 12:37 PM by Unknown No comments

Kashfa ya uchotaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow
inayoendelea kulitingisha Taifa, jana ilitawala mahubiri ya Sikukuu ya Krismasi
katika makanisa mbalimbali nchini, viongozi wa dini wakionyesha kutoridhishwa
na maelezo na hatua zinazochukuliwa.
Wakihutubia waumini wao, viongozi hao walitumia siku hiyo
kukemea vitendo vya ufisadi, wizi na uzembe.
Hofu ya Escrow
Ujumbe wa Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) wa
Kanisa la Anglikana, Dk Dickson Chilongani ulilenga kueleza hofu ya wananchi
kutokana na sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, ugumu wa maisha, ukosefu wa
ajira, kukosa uhakika wa huduma bora za matibabu na elimu pamoja na wimbi la
viongozi waandamizi wasiokuwa waaminifu na waadilifu.
Akihubiri katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu mjini Dodoma,
Askofu Chilongani alisema mbali na maisha ya ufukara na ukosefu wa huduma,
sakata la Escrow na hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa Jumatatu vimezidi
kuzidisha hofu kwa Watanzania na kuwafanya waonekane kama hawana tumaini.
Akitumia mtindo wa kuhoji, Askofu Chilongani alianza kwa kuhoji,
“Kitu gani kinakutia hofu unaposherekea sikukuu hii, watu wengi tunaishi katika
ulimwengu wa hofu kutokana na ufukara, ukosefu wa huduma, tunajiuliza
tutawasomeshaje watoto wetu, tutapataje huduma bora za matibabu, yaani kila
mmoja wetu ana hofu,” alisema.
Askofu Dk Chilongani alisema ingawa kila mtu ana hofu yake
lakini sakata la akaunti ya Escrow limejenga hofu kwa mwananchi, kila mmoja
akihoji na kutengeneza majibu yake jambo linalotoa picha kuwa jibu sahihi
halijatolewa au kupatikana.
“Mimi siyo mwanasiasa wala mtaalamu wa masuala ya siasa lakini
kuna hili sakata la Escrow ambalo juzijuzi Rais amelitolea ufafanuzi, hili nalo
linazidi kuwajengea wananchi hofu, wengine wanakosoa maazimio ya Bunge, wengine
wanataka Serikali itoe maamuzi yenye tija kwa umma, yaani ni hofu tu,” alisema.
Escrow ni fedha za umma
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo alisisitizia
kuwa fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow ni mali ya umma
kutokana na taarifa iliyowasilishwa na PAC bungeni.
Kauli hiyo inakuja baada ya Rais Kikwete kusema fedha hizo ni
mali Kampuni ya IPTL na zilikuwa Sh202 bilioni na si Sh306 bilioni kama
inavyodaiwa.
Akihubiri katika kanisa hilo jana, Lusekelo maarufu kama ‘Mzee
wa Upako’ alisema: “Niliisikiliza kwa makini mwanzo hadi mwisho (hotuba ya
Rais) leo nimeona niseme machache kwamba fedha hizo ni mali ya umma. Mimi
siungani na hao wanaodai fedha hizi siyo za umma lakini kwa hali hii hakuna
jinsi inabidi tumwachie Mungu maana yeye ndiye atakayeweza kutuvusha kutoka
hapa tulipo,” alisema.
Padri: Viongozi wa dini waliotajwa wajipime
Paroko wa Parokia ya Mugumu, Serengeti, Padri Aloisi Magabe
amesema viongozi wa dini ambao wametajwa kuhusika na fedha kwenye Akaunti ya
Tegeta Escrow wanatakiwa kujipima kwa kuwa maadhimisho ya Krismasi yana maana
kubwa, hivyo kuwa sehemu ya watu wanaotuhumiwa si jambo jema.
Akihutubia katika ibada ya Krismasi, Padri Magabe alisema
vitendo hivyo vinazidi kushika kasi lakini hatua hazichukuliwi.
Alisema ufisadi ulijichomoza kwa nguvu kwenye Richmond, Epa na
sasa Escrow, huku viongozi wa dini wakihusika, hatua ambayo ni hatari huku
akisema juhudi za kuwashughulikia wahusika huchukua muda mrefu, chanzo kikiwa
ni kulindana na rushwa. “Sina hofu ya kusema waziwazi matukio kama hayo,
nimefuatilia magazeti jinsi wanavyojitetea, bado kuna haja ya kuwa wazi zaidi,
maana nchi yetu ni ya haki na usawa, tutaupataje usawa kwa ‘skendo’ kama hizi?”
Askofu Mkude: Nina imani kubwa na JK
Askofu wa Jimbo la Morogoro, Telesphol Mkude amesema ana imani
kubwa na Rais Kikwete kwa namna anavyolishughulikia suala la kuwajibisha
waliotajwa katika sakata la Tegeta Escow na kuwaomba Watanzania kumpa muda wa
kutosha ili aweze kuendelea kutoa uamuzi ulio sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa katika ofisi ndogo
ya Kanisa Kuu la Mt Patrick, Mkude alisema suala la Escrow limepita katika
mchakato mrefu na baadhi ya wameanza kuchukuliwa hatua, wakiwamo Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema aliyejiuzulu na Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo Makazi, Profesa Anna Tibaijuka aliyefukuzwa.
“Haya mambo yanaenda na uchunguzi, sidhani kama Rais anaweza
kutoa uamuzi pasipo kujiridhisha, pamoja na kuwapo kamati iliyojiridhisha na
uchunguzi na kubaini uchotaji wa fedha za umma, lakini na yeye kwa nafasi yake
anapaswa kujiridhisha kupitia jopo lake,” alisema Askofu Mkude.
Hofu ya Mungu na ufisadi
Hofu ya Mungu imeelezwa kuwa ndiyo pekee itakayoondoa wizi na
ufisadi miongoni mwa viongozi na watendaji badala ya kutegemea sheria pekee.
Hayo yalisemwa jana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa wakati akihubiri katika ibada ya
Krismasi katika Kanisa la Azania Front, jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo inafanana na ile iliyotolewa na Mchungaji Kiongozi wa
Kanisa la Gloryland International la jijini Tanga, Manase Maganga.
Malasusa alisema kutokuwapo kwa hofu ya Mungu miongoni mwa
Watanzania, ndiyo sababu ya kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi.
“Wakristo tunahitaji kusimama kwa ujasiri na kukemea mabaya yote
katika jamii yetu hata kama yanafanywa na marafiki zetu kwa kuwa neno
linatuagiza kufanya hivyo. Bwana anasema ‘woga ni dhambi’, hivyo tuwe makini
ili kuepuka dhambi hii yenye madhara kwa watu wengi katika Taifa hili,”
alisisitiza Dk Malasusa.
Vijana na siasa
Askofu Evarist Chengula wa Jimbo Katoliki Mbeya akiwataka vijana
kujitosa kwenye siasa ili kuondoa giza nene ambalo limetawala katika nchi.
“Vijana mliopo ndani humu leo, mshughulike na siasa kwa kuingia
katika chama ambacho mnaona kitachochea amani, utulivu, uvumilivu, ustahimilivu
miongoni mwa wafuasi wenu lakini siyo chama kinachowakumbatia mafisadi,
wabinafsi na wenye kujilimbikizia mali na kitakachosababisha chokochoko yoyote
ya kutoweka kwa amani,” alisema Askofu Chengula bila kutaja jina la chama
hicho.
Aliongeza: “Furaha imetoweka miongoni mwa Watanzania na furaha
tunayoizungumzia hapa siyo kunywa, kucheza na kula, bali ni kuwa na amani,
utulivu ndani ya mioyo yetu. Kutoweka kwa amani si lazima watu wapigane vita na
damu imwagike, hapana, hata wale walioko maofisini wanaposhindwa kutimiza
wajibu wao, mtu akabaki akinung’unika moyoni mwake huo ndiyo mwanzo amani wa
kutoweka.
Tatizo uongozi mbovu
Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Tarcisius Ngalalekumtwa
amesema umaskini unaolikabili Taifa kwa sasa unatokana na sera mbovu za nchi
pamoja na uongozi mbovu.
Ngalalekumtwa ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania (TEC), alitoa kauli hiyo katika ibada ya Krismasi huku akisisitiza
kuwa Taifa la Tanzania linao utajiri mkubwa unaoweza kuwasaidia wananchi wake
kuishi bila ya matatizo.
“Tanzania siyo nchi maskini, bali kinachosababisha iwe hivyo ni
sera mbovu zilizopo na uongozi mbovu. Hivi kweli sisi hatuna mahali pa
kuwahifadhi watu wetu? Ardhi? (waumini wakajibu tunayo), madini? (tunayo)
misitu? (tunayo), mahindi? (tunayo), unawezaje kusema Taifa hili ni maskini?
“Mimi nimekuwa nikishangaa na hata ninyi mmesikia haya mabilioni
ya fedha unayochukua mtu mmoja utakula hadi lini, umaskini tulionao unatokana
na mtu mmoja kula chakula kinachoweza kuliwa na watu zaidi ya milioni moja,
katika mazingira kama hayo ni lazima watu wengine wawe maskini,” alisema.
Uchaguzi wa mitaa
Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine Niwemuguzi aliwataka
waumini wa Kikristo na watu waliopewa nafasi za utendaji kuwa wavumilivu na
kuwajibika bila kuwakwaza wenzao.
Akihubiri katika ibada ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa la
Mt. Francisco wa Asiz, Parokia ya Ngara Mjini, juzi usiku, Askofu Niwemugizi
aliwataka waumini kutimiza wajibu wao wakitanguliza subira, kutokata tamaa na
kuwa makini kuzikabili changamoto za dunia.
Katika mahubiri hayo, askofu huyo ambaye pia ni Makamu wa Rais
wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), alisema uchaguzi wa Serikali za Mitaa
uliomalizika hivi karibuni, haukufanyika vizuri kama ilivyotarajiwa, taratibu
zilivurugwa na tathmini yake inatia shaka.
Kutenda haki mwakani
Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Dar es Salaam,
Padri Stephano Kaombe aliwataka Watanzania kuacha woga wanapotekeleza majukumu
yao na kuhakikisha wanafanya mambo hayo kwa kiasi na haki.
Katika mahubiri yake ya dakika 15 kwenye mkesha wa Krismasi
kitaifa juzi usiku, Padri Kaombe alisema waumini wanafunzwa kuwa watenda haki
na katika mwaka ujao ambao utakuwa na mambo mengi yanayohitaji kiasi na haki.
“Tunapoalikwa kwenye daftari la wapigakura tutende haki, katika
kuipigia kura ya maoni Katiba Inayopendekezwa tutende haki, tunapofanya
uchaguzi napo tutende haki na tunaweza kuyafanya hayo iwapo tutakuwa na kiasi
na hatuna woga.”
Viongozi na amani
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF),
Zachary Kakobe amesema hatakuwa tayari kuhubiri amani inayoshinikizwa na
viongozi wa Serikali wakati wao ndiyo wanaoivuruga: “CCM imekuwa na hofu ya
kuondolewa madarakani, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulikuwa umejaa
ujanjaujanja na hata kuwafukuza wakurugenzi ni kiini macho.”
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Anglikana, St Albano, Aidano
Mbulinyingi akihubiri katika mkesha wa Krismasi aliwataka Watanzania kuwaombea
viongozi wa nchi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
“Tusiwe na vinyongo, tukunjue mioyo yetu tuwaombee Rais,
mawaziri na viongozi wengine ili Taifa liendelee kuwa na amani na utulivu,”
alisema Mbulinyingi na kusisitiza kuwa bila kuwaombea hawawezi kutekeleza
majukumu yao ipasavyo.
Akizungumza kwenye ibada ya misa iliyoadhimishwa katika Kanisa
Katoliki la Mtakatifu Joseph, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam,
Eusebius Nzigilwa alitoa wito kwa jamii kusherehekea sikukuu hii kwa upendo na
amani bila kuwasahau watu wasiojiweza ili na wao wajisikie kuwa ni sehemu ya
jamii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Search
Translate
Popular Posts
-
Leo wanawake wenzangu kwenye safu yetu hii pendwa nimewaletea mada moja nzito ambayo ukiiendekeza unavunja nyumba yako hivihivi unajiona.H...
-
Utandawazi utawaabisha wengi kwani hizi simu zetu ukizubaa kidogo mtu anakupiga picha hata kama hujadhamiria kufanya hivi.
-
Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela AIBU ilioje! Denti wa chuo kimoja jijini Dar, anayefahamika kwa jina moja la Martha, amepiga...
-
Hebu niambie...umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi, umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? ...
-
Wanachuo wazidi kuwa mfano mbaya licha kuonekana wasomi na ndio tegemeo kwa taifa la kesho lakini cha ajabu wanazidi kufanya madudu badal...
-
MDADA MWENYEWE NI HUYU. DENT mmoja katika Chuo Kikuu kimojawapo hapa nchini amepiga picha zisizo na maadili akiwa na njemba wake katika ...
-
Kweli dunia inamambo watu kadhaa wamekamatwa na kamera zetu wkingonoka bila uoga wowote tena hadharani hebu ona picha hapa
-
Hivi Majuzi mke wa Mchungaji mmoja amekamatwa laivu akingonoka vichakani umbali kidogo kutoka katika nyumbani kwake Mke wa Mchungaji a...
-
Polisi mkoani Tanga wamesema wataendesha msako wa kuwakamata watu wanaofanya biashara ya ngono katika nyumba za starehe na mitaa maarufu ...
Blog Archive
-
▼
2014
(168)
-
▼
December
(168)
- BAADA YA KIMYA CHA MUDA MREFU MREMBO RAYUU AIBUKA ...
- Polisi Yatangaza Msako kwa Wanawake Wanaofanya Bia...
- Nimeamua Kutoka Kimapenzi na Binti wa Kazi ( Hausi...
- Samantha Apokelewa Kwa Mikono Miwili na Familia ya...
- PHOTO’S: HIVI NDIVYO ALIVYOPOKELEWA DIAMOND NA KUN...
- SIMBA YAFUKUZA MAKOCHA
- DIAMOND PLATNUMZ ATUA RWANDA KWA SHANGWE
- WAIMBA INJILI WANA NINI?
- MWANAMKE ADAIWA KUTEKA WATOTO
- BASTOLA TISHIO DAR!
- VANESSA AWATOA KIMASOMASO WASANII WA KIKE
- Bilionea wa Nigeria ampiku Oprah na kuwa mwanamke ...
- Mvua Yaua Jijini Dar.....Mtoto Asombwa na Maji aki...
- Binti Ajizalisha na kutumbukiza mtoto kwenye ndoo
- Mgombea urais atabiriwa kifo.....Yadaiwa Atafariki...
- Washitakiwa mauaji ya Dk Mvungi wazua kizaazaa mah...
- Hili ni Fundisho Kwa Wanaume Wanaopenda Kutongoza ...
- MAKAVU LIVE!!!:: UTAMU WA MUA UKIKUTANA NA KIFUNDO...
- Wajua Jinsi ya Kumdhibiti Mpenzi Anayepiga Mizinga?
- PICHA ZA UTAMU ZA DENTI WA CHUO KIKUU CHA UDOM ZAN...
- Bi dada... Utafanya nini? Mmeo Anatembea na binti ...
- Waziri Nyalandu atangaza nia ya kuwa Rais wa Tanzania
- Kashfa ya Escrow ndo sababu kuu ya Anguko la CCM-W...
- Tibaijuka: Nitagombea Ubunge Mwakani licha ya Saka...
- Mwenyekiti wa CHADEMA Atimuliwa nchini kwa madai k...
- UCHAWI:BIBI KIZEE AKUTWA KAANGUKA NJE YA KANISA AS...
- TAZAMA JINSI SIKUKUU YA KRISMAS INAVYOENDELEA KATI...
- BAADA YA KIMYA KIREFU MSANII 'Q CHIEF' SASA KUACHA...
- LAANA YA SIKU : :VIJANA WAFANYA USHENZI KUPITILIZA
- LAANA..!!! BOFYA UONEE VIZURII DADA HUYU ALIVYOAMU...
- PICHA ZA UCHI ZA MSANII MAARUFU WA KIKE AKILIWA TI...
- ZAIDI YA LAANA: HUU NDIOUCHAFU ULIOFANYIKA JANA KW...
- RAIS OBAMA AITWA TUMBILI NA KOREA KASKAZINI!
- DAVINA:STEVE NYERERE NI MTU POA ILA ANA VIMATATIZO...
- DIAMOND PLATNUMZ HANA UWEZO WA KUMPA MWANAMKE UJAU...
- KAKA NA DADA WANASWA LAIVU WAKIFANYA MAPENZI,WAFAN...
- MAJANGA !!! MKE WA MTU AWEKA PICHA CHAFU KATIKA UK...
- WASTARA KUMUANIKA MRITHI WA SAJUKI
- Hizi Ndizo Sifa Za Mtu Anayefaa Kuwa Rais Ajaye ,W...
- Dunia Imeisha Tizama Picha Za Hawa Wadada Walizopo...
- DAVIDO ALA DENDA NA SHABIKI AKIWA STEJINI!!!
- DUNIA IMEKWISHA CHEKI PICHA YA MCHUMBA WA MTU AKIN...
- AFARIKI DUNIA BAAADA YA KULIPULIWA NA BOMU ALILOTA...
- HILI NI FUNDISHO KWA WAKE ZA MARAISI AFRIKA!!!HUYU...
- LIPUMBA NA ZITTO KABWE WAPANGA KUWASHA MOTO WA ESC...
- HIVI NDIVYO TIBAIJUKA ALIVYOTEMA CHECHE HUKO JIMBO...
- HIVI UNAFAHAMU KUWA LIPUMBA ALISHAWAHI KUWA MSAIDI...
- BUBU Afanyiwa Unyama wa Kutisha......Wanaume Watan...
- Hausiboi Aliyelawiti Mtoto wa Miaka 6 Ahukumiwa Ki...
- BAKWATA Yasisitiza kuwa Maamuzi ya Rais Kikwete ku...
- Matokeo Mabaya ya CCM Singida: Nyalandu Abebeshwa ...
- HII NI NOMA..!! JIONEE PICHA 15 ZA HUYU MZUNGU ALI...
- JINSI YA KUJIZUIA USIKOJOE MAPEMA NA HIVYO KUSHIND...
- Krismasi ni Escrow kila kona
- Vijana Watatu Wakamatwa Wakijaribu Kuiba Sanamu ya...
- Rais Kikwete atakiwa kuwachukulia hatua Mawaziri W...
- CCM yaongoza matokeo ya jumla serikali za mitaa
- Ukawa Mkilifanya Hili, 2015 Mnashinda kwa Zaidi ya...
- Ray C: Nina uhakika Alikiba Akipata Support ya Dia...
- Panapo Fuka Moshi Kuna Moto..Habari za Millard Ayo...
- Bifu la Davido na Wizkid Limeisha, La Ally Kiba na...
- Sserunkuma atupia mbili, aonyesha cheche Zenji
- SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIK...
- VODACOM TANZANIA ILIVYOWARUSHA WATEJA WAKE KILA KO...
- Waziri Muhongo aanza Ziara ya Siku 6 Mkoani Mara k...
- MADAWA YA KULEVYA HATARI ZAIDI KWA WASANII
- KUNDI LILILOPATA PIGO ZAIDI 2012-14
- SHOO YA DIAMOND DAR LIVE YAACHA HISTORIA
- R.I.P WASANII WETU! KINACHOWAUA KWA KASI CHAJULIKANA
- FAIZA: MIMI SIYO MBULULA KWA KUVAA PEMPASI
- BALAA LA KRISMASIMREMBO APOTEZA FAHAMU
- DUH!! JE WAJUA KILICHOMPATA MENEJA WA CLOUDS JUU Y...
- AIBU YA MWAKA!!!!!! TAZAMA ALICHOFANYIWA DADA HUYU...
- PICHA ZA WATU WAZIMA WAKINGONOKA HADHARANI HII NI ...
- TAMASHA LA TUONANE JANUARY (TUO8 JANUARY) LAFANA M...
- JINSI YA KUMTOA MWANAMKE BIKRA BILA MAUMIVU ........
- Diamond Aeleza Demu Aliemtungia Wimbo Wake Mpya Wa...
- Ona Mama Diamond Jinsi Anavoonekana Kuwa Chanzo Ch...
- FUMANIZI!!! PATA KUONA ALICHOFANYIWA DADA HUYU BAA...
- MJUE MKE MTARAJIWA WA MASANJA MKANDAMIZAJI!, IONE ...
- WANACHUO WANAOPIGA PICHA ZA UTUPU WAZIDI KUONGEZEK...
- Baadhi ya Picha za Wema na Van Vicker Wakiwa Katik...
- Nimeamini, Mabinti wa Kichaga Hawajui Mapenzi Hata...
- Wavulana Ma-handsome Hawana Lolote Kitandani..Kazi...
- Yamenikuta: Mchumba wangu amezaa angali bikra
- Rais Kikwete Akutana na Msanii Diamond Platnumz Ik...
- JOKATE: SIJAWAHI KUROGA ILI NIFANIKIWE
- WEWE TIBAIJUKA! JEMBE LISILOLIMA LINA FAIDA GANI?
- DIAMOND AANIKA SABABU 5 ZA KUMPENDA ZARI!
- Wema Sepetu Apandishwa Kizimbani
- Mume Ajinyonga Ukweni baada ya Mkewe Kumkataa
- Baada ya Kupotea Kwa Muda Mrefu Agness Masogange A...
- Headmistress Caught Being Banged By Her Watchman I...
- Wema Ampongeza Jokate Lakini Asisitiza Kuendelea K...
- Magazeti ya Leo Jumatatu ya tarehe 22 Disemba 2014
- Mke wa Mtu Anaswa Akijiuza Kusaka Pesa za Christmass
- Diamond: Aliyenifundisha Kuongea Kiingereza ni Pen...
- CHADEMA Watoa Tahadhari kwa Rais kuhusu Kuwatetea ...
- MTOTO WA JACKIE CHAN ASHITAKIWA KWA DAWA ZA KULEVYA
- MWENYEKITI WA PROIN, JOHNSON LUKAZA NA MDOGO WAKE ...
-
▼
December
(168)
0 comments:
Post a Comment