Thursday, December 25, 2014

On 10:37 PM by Unknown   No comments
MAANDIKO yanatueleza kwamba, kila nafsi itaonja mauti hilo halina ubishi. Tunafurahia pumzi aliyotupa Mungu lakini tunatambua kabisa ipo siku ataichukua, uhai utatoweka na biashara yetu duniani inakuwa ndiyo imeishia hapo.
Wakati tukilitafakari hilo na tukitambua kabisa kazi yake Mola haina makosa, si vibaya tukiwakumbuka baadhi ya wasanii waliotutoka hususan katika miaka ya hivi karibuni.
VIFO VINAONGEZEKA
Kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele, ndivyo vifo vinaonekana kuongezeka nchini. Miaka ya nyuma ilikuwa ni nadra sana kusikia kifo cha msanii lakini miaka ya hivi karibuni imekuwa si kitu cha kushtua sana.
Ukitazama orodha ya vifo vya wasanii kwa ujumla Bongo vilivyotokea ndani ya miaka miwili iliyopita, utagundua hesabu yake haipungui 30 lakini kabla ya hapo vifo vilikuwa ni vya kuhesabu. Kuna kitu cha kutafakari zaidi hapa.
WASANII WA MUZIKI WALIOFARIKI
Wasanii wa muziki waliofariki 18 ambao ni Mangwea, Langa, Mzee Gurumo, Bi Kidude, Shemi, Aisha Madinda, Abuu Semhando, MCD, Amigolous, Joseph Maina, Mariam Hamis, Geez Mabovu, Mpogo, YP, Amina, Nyawana, Olida, Debora na  Aisha Madinda.
WASANII WA FILAMU
Upande wa wasanii wa filamu ni 13 ambao ni Kanumba, Tyson, Sharo Milionea, Kuambiana, Mzee Small, John, Mlopelo, Sajuki, Manento, Sherry, Recho Haule, Kashi, Melissa na Benny.
TWANGA PEPETA PIGO ZAIDI
Ukiachana na kundi hilo, katika wanamuziki Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ iliyo chini ya mkurugenzi wake, Asha Baraka, ndiyo iliyopata pigo zaidi kwani ndani ya miaka miwili, imeondokewa na wanamuziki wake wanne.
Ameondoka mpiga tumba maarufu, Sudi Mohamed ‘MCD’ (maradhi), mwimbaji mkongwe, Hamis Kayumbu ‘Amigolous’ (maradhi ya moyo), mpiga drums, Abuu Semhando (ajali) na mnenguaji Aisha Madinda (haijajulikana).
USHAURI
Ni vyema wasanii pamoja na watu wengine tukamrudia Mungu, tukajenga utaratibu wa kujua afya zetu mara kwa mara na kuepuka ajali zisizo za lazima kwa kufuata sheria za usalama barabarani.

0 comments:

Post a Comment