Monday, December 22, 2014

On 8:22 AM by Unknown   No comments


Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza.
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imewachia huru Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza na mdogo wake Mwesiga Lukaza waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa shilingi bilioni sita katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu (EPA), baada ya kuwaona hawana hatia.
Hukumu hiyo Imetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu, Edson Mkasimongwa aliyekuwa akisaidiana na Hakimu Mkazi, Pamela Mazengo.
Johnson Lukaza ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), alikuwa akitetewa na Wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwa na Wakili Alex Mshumbusi.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mkasimogwa alisema kesi hiyo ya mwaka 2008, Mahakama imesikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kupitia vielelezo mbalimbali. Mahakama yake imefikia uamuzi wa kuwaachia huru washitakiwa wote wawili kwa sababu upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi thabiti ambao ungeishawishi mahakama hiyo iwakute na hatia washitakiwa hao.

0 comments:

Post a Comment