Monday, December 22, 2014
On 8:30 AM by Unknown No comments

C/HQ/ADM/PRESS/37 21/12/2014
Ndugu waandishi wa habari,
Tumewaita hapa baada ya kupata fununu kuwa Rais Jakaya Kikwete
anataka kutumia hotuba yake ya kesho( leo ) na wanaoitwa, “Wazee wa Dar es
Salaam” kutetea wizi mkubwa wa fedha za umma uliofanyika ndani ya Benki Kuu
(BoT), kupitia Akaunti ya Tegeta Escrow.
Tunazo taarifa kuwa Rais Kikwete amejipanga kuuhadaa umma kwa
kisingizio cha uchunguzi wa Ikulu, ili kuwalinda watuhumiwa ambao wanapaswa
kuwajibishwa kwa kuwafuta kazi, kushitakiwa na kufirisiwa. Habari tulizozipata
kutoka ndani ya Ikulu kwenyewe, zinasema Rais Kikwete amejiandaa kumlinda
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara
hiyo, Eliakim Maswi.
Tunapenda kumtahadharisha Rais Kikwete kuachana mara moja na
mpango wowote wa kumlinda Profesa Muhongo na Maswi, ambao hadi muda huu
walipaswa siyo kuwa nje ya ofisi, bali walitakiwa kuwako gerezani.
Ndugu waandishi wa habari;
Ndugu waandishi wa habari;
Umma unafahamu kwamba anayejiita mmiliki wa kampuni ya PAP,
alikabidhiwa fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Escrow, kabla ya kuwa mmiliki
halali wa kampuni hiyo.
Ushahidi wa hili, unapatikana katika kesi iliyofunguliwa
Mahakama Kuu ya Tanzania na James Rugamalira, dhidi ya Gavana wa Benki Kuu
(BoT), Prof. Benno Ndulu, kampuni ya PAP na Benki ya Stanbic, tawi la Tanzania.
Rugamalira alifungua shauri hili baada ya kukuta fedha
zilizokuwapo kwenye akaunti ya Escrow zimeshachukuliwa, wakati yeye akiwa bado hajamaliziwa
kiasi chake cha fedha alichokuwa anadai baada ya kuuza asilimia 30 ya hisa zake
katika IPTL.
Katika shauri hilo lililomalizika kwa njia ya usuluhishi wa
mahakama, Mahakama Kuu ya Tanzania, pamoja na mengine, ilisema yafuatayo:
·
Kwamba baada ya
kampuni ya VIP kulipwa fedha zake zilizotajwa katika mkataba, itailipa Mamlaka
ya Mapato ya Tanzania (TRA) kodi yote ya mapato inayotokana na mkataba
inayofikia Sh. 38, 186,584,322/- (bilioni thelathini na nane milioni mia moja
na themani na sita laki tano na elfu themanini na nne na mia tatu ishirini na
mbili) kama zilivyokadiriwa na TRA kupitia Kadirio la Kodi Na. 427038820 la
tarehe 15 Januari 2014. Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani tarehe 8 Januari
2014 na VIP ENGINEERING AND MARKETING LIMITED (VIP) kama mdai na iliunganisha
kesi za madai Na. 49/ 2002 na kesi ndogo Na. 254 YA 2003.
·
Kwamba
baada ya VIP kulipa kodi hiyo kwa TRA, fedha zake zilizobaki hazitalipwa kwake
mpaka pale itakapowasilisha Cheti cha Kulipa Kodi na hati za kuhamisha asilimia
30 ya hisa zake katika IPTL kwa mwanasheria wa PAP, na wasilisho hilo
lilitakiwa kufanyika kabla ya saa 10 jioni ya tarehe 27 Januari 2014.
·
Aidha, baada ya
kulipwa kiwango chote cha mkataba kilichotajwa hapo juu, VIP itathibitisha
uridhiaji na ukubali wake wa kuhamishwa asilimia 70 ya hisa za MECHMAR
CORPORATION (MALAYSIA) BERHAD katika IPTL, na uridhiaji na ukubali huo
unarudishwa nyuma kuanzia tarehe ya mauzo na uhamishaji wa hisa hizo kwa PAP.
Ndugu waandishi wa habari;
Hii maana yake nini? Jibu ni kwamba, wakati PAP analipwa kiasi
cha Sh. 321 bilioni kutoka BoT, haikuwa mmiliki halali wa IPTL. Hakuwahi
kusajili hisa zake BRELA wala hakuwa amenunua asimia 30 ya hisa za VIP.
Huu ni wizi ambao hauwezi kuvumiliwa na umma na chama chetu,
ambacho ni tegemeo la Watanzania katika kulinda rasimaliza za taifa, ikiwamo
fedha na kutetea haki za wanyonge na kusimamia misingi ya uwajibijkaji,
hakiwezi kunyamaza na kumuacha Rais Kikwete akitekeleza mradi wake wa kulinda
wezi. Hakiwezi!
Kwa msingi huo, tunamtaka Rais Kikwete katika hotuba yake ya
kesho( leo), kuwajibisha wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine,
katika kutekeleza wizi huo.
Miongoni mwao, ni Prof. Muhongo, Maswi, Gavana wa BoT, Prof.
Ndulu, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Silviacius Likwelile, Waziri wa Fedha,
Saada Mkuya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredric Werema na Mkurugenzi
Mkuu wa Tanesco, Felicesmi Mramba.
Ndugu waandishi wa habari,
Watanzania bado wanakumbuka kauli iliyotolewa bungeni wakati wa
mkutano uliopita kuwa familia ya Rais Kikwete nayo iko nyuma ya sakata hili
ikiwa mnufaikaji mkubwa kupitia kwa mtu aitwaye Albert Marwa ambaye ana
uhusiano na familia hiyo.
Kitendo cha Rais Kikwete kushindwa kuchukua hatua madhubuti
katika jambo hili, utakuwa ni ushahidi wa wazi kuwa kigugumizi ambacho kimekuwa
kikiikabili serikali yake katika jambo hili kinasukumwa na jambo kubwa nyuma
yake, ikiwamo kujilinda binafsi na kulinda familia yake.
Ndugu waandishi wa habari,
Suala la miamala iliyofanyika kupitia Benki ya Stanbic katika
sehemu ya kashfa hiyo ya Akaunti ya Escrow, si suala la kufanyia mzaha au
kupuuzwa hata kidogo katika ufisadi huu.
Ni kupitia benki hiyo ndiko kiwango kikubwa cha fedha zaidi ya
Sh. 160 bilioni, zilibebwa kwa magunia, malumbesa na sandarusi ndani ya siku
moja mchana kweupe, tena tunaambiwa wengine walikwenda kwa magari yenye nambari
za serikali na fedha hizo zilipelekwa Ikulu ambako Rais Kikwete anafanyia kazi
na kuishi.
Ni ukweli ulio wazi kuwa hakuna benki ndani ya nchi yetu
inayoweza kufanya miamala ya mabilioni ya fedha kwa kiwango hicho, bila BoT
kuidhinisha. Kwa mantiki hiyo hiyo, Gavana Prof. Ndulu hawezi kukwepa
uwajibikaji kwenye jambo hili zito kwa kuwa alilifahamu na kulilidhia.
Tunatarajia Rais Kikwete ataueleza umma wa Watanzania hatua
zilizochukuliwa dhidi ya watumishi hawa wa umma na siyo kuja na visingizio vya
miamala iliyochukuliwa katika Benki ya Mkombozi.
Watanzania wanasubiri kusikia Rais Kikwete anachukua hatua dhidi
ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum ambaye wakati fedha katika Akaunti ya
Escrow zinatolewa kati ya Septemba na Desemba mwaka jana, alikuwa ndiye Kaimu
Waziri wa Fedha.
Wakati huo, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa
alikuwa katika matibabu ya ugonjwa uliopelekea kifo chake ambacho kimedaiwa
kuwa na utata, nchini Afrika Kusini.
Ndugu waandishi wa habari;
Aidha, katika kuwatafuta watu waliochukua fedha za Akaunti ya
Escrow kwa magunia na malumbesa, Rais Kikwete aweke wazi kile kinachoonekana
ushirika wa ufisadi kati ya serikali, Benki ya Stanbic na chama chake – Chama
Cha Mapinduzi (CCM), kupitia Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulahman Kinana.
Tunazo taarifa za uhakika kwamba Kinana alikuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Benki hiyo na Mjumbe wa Bodi ya Stanbic, na ambaye alikuwa kiunganishi
kikubwa kati ya serikali, CCM na Benki katika kufanya miamala ya aina hiyo ya
kifisadi.
Rais Kikwete anatarajiwa kumwagiza Kinana awataje watu
waliokwenda kuchukua mabilioni ya fedha kwa malumbesa, magunia na sandarusi,
vinginevyo atakuwa anahalalisha madai haya kuwa ushirikiano huu si bahati mbaya
na ndiyo maana, fedha kutoka Akaunti ya Escrow ya Tegeta, zilipitia katika
benki hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Search
Translate
Popular Posts
-
Leo wanawake wenzangu kwenye safu yetu hii pendwa nimewaletea mada moja nzito ambayo ukiiendekeza unavunja nyumba yako hivihivi unajiona.H...
-
Utandawazi utawaabisha wengi kwani hizi simu zetu ukizubaa kidogo mtu anakupiga picha hata kama hujadhamiria kufanya hivi.
-
Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela AIBU ilioje! Denti wa chuo kimoja jijini Dar, anayefahamika kwa jina moja la Martha, amepiga...
-
Hebu niambie...umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi, umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? ...
-
Wanachuo wazidi kuwa mfano mbaya licha kuonekana wasomi na ndio tegemeo kwa taifa la kesho lakini cha ajabu wanazidi kufanya madudu badal...
-
MDADA MWENYEWE NI HUYU. DENT mmoja katika Chuo Kikuu kimojawapo hapa nchini amepiga picha zisizo na maadili akiwa na njemba wake katika ...
-
Kweli dunia inamambo watu kadhaa wamekamatwa na kamera zetu wkingonoka bila uoga wowote tena hadharani hebu ona picha hapa
-
Hivi Majuzi mke wa Mchungaji mmoja amekamatwa laivu akingonoka vichakani umbali kidogo kutoka katika nyumbani kwake Mke wa Mchungaji a...
-
Polisi mkoani Tanga wamesema wataendesha msako wa kuwakamata watu wanaofanya biashara ya ngono katika nyumba za starehe na mitaa maarufu ...
Blog Archive
-
▼
2014
(168)
-
▼
December
(168)
- BAADA YA KIMYA CHA MUDA MREFU MREMBO RAYUU AIBUKA ...
- Polisi Yatangaza Msako kwa Wanawake Wanaofanya Bia...
- Nimeamua Kutoka Kimapenzi na Binti wa Kazi ( Hausi...
- Samantha Apokelewa Kwa Mikono Miwili na Familia ya...
- PHOTO’S: HIVI NDIVYO ALIVYOPOKELEWA DIAMOND NA KUN...
- SIMBA YAFUKUZA MAKOCHA
- DIAMOND PLATNUMZ ATUA RWANDA KWA SHANGWE
- WAIMBA INJILI WANA NINI?
- MWANAMKE ADAIWA KUTEKA WATOTO
- BASTOLA TISHIO DAR!
- VANESSA AWATOA KIMASOMASO WASANII WA KIKE
- Bilionea wa Nigeria ampiku Oprah na kuwa mwanamke ...
- Mvua Yaua Jijini Dar.....Mtoto Asombwa na Maji aki...
- Binti Ajizalisha na kutumbukiza mtoto kwenye ndoo
- Mgombea urais atabiriwa kifo.....Yadaiwa Atafariki...
- Washitakiwa mauaji ya Dk Mvungi wazua kizaazaa mah...
- Hili ni Fundisho Kwa Wanaume Wanaopenda Kutongoza ...
- MAKAVU LIVE!!!:: UTAMU WA MUA UKIKUTANA NA KIFUNDO...
- Wajua Jinsi ya Kumdhibiti Mpenzi Anayepiga Mizinga?
- PICHA ZA UTAMU ZA DENTI WA CHUO KIKUU CHA UDOM ZAN...
- Bi dada... Utafanya nini? Mmeo Anatembea na binti ...
- Waziri Nyalandu atangaza nia ya kuwa Rais wa Tanzania
- Kashfa ya Escrow ndo sababu kuu ya Anguko la CCM-W...
- Tibaijuka: Nitagombea Ubunge Mwakani licha ya Saka...
- Mwenyekiti wa CHADEMA Atimuliwa nchini kwa madai k...
- UCHAWI:BIBI KIZEE AKUTWA KAANGUKA NJE YA KANISA AS...
- TAZAMA JINSI SIKUKUU YA KRISMAS INAVYOENDELEA KATI...
- BAADA YA KIMYA KIREFU MSANII 'Q CHIEF' SASA KUACHA...
- LAANA YA SIKU : :VIJANA WAFANYA USHENZI KUPITILIZA
- LAANA..!!! BOFYA UONEE VIZURII DADA HUYU ALIVYOAMU...
- PICHA ZA UCHI ZA MSANII MAARUFU WA KIKE AKILIWA TI...
- ZAIDI YA LAANA: HUU NDIOUCHAFU ULIOFANYIKA JANA KW...
- RAIS OBAMA AITWA TUMBILI NA KOREA KASKAZINI!
- DAVINA:STEVE NYERERE NI MTU POA ILA ANA VIMATATIZO...
- DIAMOND PLATNUMZ HANA UWEZO WA KUMPA MWANAMKE UJAU...
- KAKA NA DADA WANASWA LAIVU WAKIFANYA MAPENZI,WAFAN...
- MAJANGA !!! MKE WA MTU AWEKA PICHA CHAFU KATIKA UK...
- WASTARA KUMUANIKA MRITHI WA SAJUKI
- Hizi Ndizo Sifa Za Mtu Anayefaa Kuwa Rais Ajaye ,W...
- Dunia Imeisha Tizama Picha Za Hawa Wadada Walizopo...
- DAVIDO ALA DENDA NA SHABIKI AKIWA STEJINI!!!
- DUNIA IMEKWISHA CHEKI PICHA YA MCHUMBA WA MTU AKIN...
- AFARIKI DUNIA BAAADA YA KULIPULIWA NA BOMU ALILOTA...
- HILI NI FUNDISHO KWA WAKE ZA MARAISI AFRIKA!!!HUYU...
- LIPUMBA NA ZITTO KABWE WAPANGA KUWASHA MOTO WA ESC...
- HIVI NDIVYO TIBAIJUKA ALIVYOTEMA CHECHE HUKO JIMBO...
- HIVI UNAFAHAMU KUWA LIPUMBA ALISHAWAHI KUWA MSAIDI...
- BUBU Afanyiwa Unyama wa Kutisha......Wanaume Watan...
- Hausiboi Aliyelawiti Mtoto wa Miaka 6 Ahukumiwa Ki...
- BAKWATA Yasisitiza kuwa Maamuzi ya Rais Kikwete ku...
- Matokeo Mabaya ya CCM Singida: Nyalandu Abebeshwa ...
- HII NI NOMA..!! JIONEE PICHA 15 ZA HUYU MZUNGU ALI...
- JINSI YA KUJIZUIA USIKOJOE MAPEMA NA HIVYO KUSHIND...
- Krismasi ni Escrow kila kona
- Vijana Watatu Wakamatwa Wakijaribu Kuiba Sanamu ya...
- Rais Kikwete atakiwa kuwachukulia hatua Mawaziri W...
- CCM yaongoza matokeo ya jumla serikali za mitaa
- Ukawa Mkilifanya Hili, 2015 Mnashinda kwa Zaidi ya...
- Ray C: Nina uhakika Alikiba Akipata Support ya Dia...
- Panapo Fuka Moshi Kuna Moto..Habari za Millard Ayo...
- Bifu la Davido na Wizkid Limeisha, La Ally Kiba na...
- Sserunkuma atupia mbili, aonyesha cheche Zenji
- SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIK...
- VODACOM TANZANIA ILIVYOWARUSHA WATEJA WAKE KILA KO...
- Waziri Muhongo aanza Ziara ya Siku 6 Mkoani Mara k...
- MADAWA YA KULEVYA HATARI ZAIDI KWA WASANII
- KUNDI LILILOPATA PIGO ZAIDI 2012-14
- SHOO YA DIAMOND DAR LIVE YAACHA HISTORIA
- R.I.P WASANII WETU! KINACHOWAUA KWA KASI CHAJULIKANA
- FAIZA: MIMI SIYO MBULULA KWA KUVAA PEMPASI
- BALAA LA KRISMASIMREMBO APOTEZA FAHAMU
- DUH!! JE WAJUA KILICHOMPATA MENEJA WA CLOUDS JUU Y...
- AIBU YA MWAKA!!!!!! TAZAMA ALICHOFANYIWA DADA HUYU...
- PICHA ZA WATU WAZIMA WAKINGONOKA HADHARANI HII NI ...
- TAMASHA LA TUONANE JANUARY (TUO8 JANUARY) LAFANA M...
- JINSI YA KUMTOA MWANAMKE BIKRA BILA MAUMIVU ........
- Diamond Aeleza Demu Aliemtungia Wimbo Wake Mpya Wa...
- Ona Mama Diamond Jinsi Anavoonekana Kuwa Chanzo Ch...
- FUMANIZI!!! PATA KUONA ALICHOFANYIWA DADA HUYU BAA...
- MJUE MKE MTARAJIWA WA MASANJA MKANDAMIZAJI!, IONE ...
- WANACHUO WANAOPIGA PICHA ZA UTUPU WAZIDI KUONGEZEK...
- Baadhi ya Picha za Wema na Van Vicker Wakiwa Katik...
- Nimeamini, Mabinti wa Kichaga Hawajui Mapenzi Hata...
- Wavulana Ma-handsome Hawana Lolote Kitandani..Kazi...
- Yamenikuta: Mchumba wangu amezaa angali bikra
- Rais Kikwete Akutana na Msanii Diamond Platnumz Ik...
- JOKATE: SIJAWAHI KUROGA ILI NIFANIKIWE
- WEWE TIBAIJUKA! JEMBE LISILOLIMA LINA FAIDA GANI?
- DIAMOND AANIKA SABABU 5 ZA KUMPENDA ZARI!
- Wema Sepetu Apandishwa Kizimbani
- Mume Ajinyonga Ukweni baada ya Mkewe Kumkataa
- Baada ya Kupotea Kwa Muda Mrefu Agness Masogange A...
- Headmistress Caught Being Banged By Her Watchman I...
- Wema Ampongeza Jokate Lakini Asisitiza Kuendelea K...
- Magazeti ya Leo Jumatatu ya tarehe 22 Disemba 2014
- Mke wa Mtu Anaswa Akijiuza Kusaka Pesa za Christmass
- Diamond: Aliyenifundisha Kuongea Kiingereza ni Pen...
- CHADEMA Watoa Tahadhari kwa Rais kuhusu Kuwatetea ...
- MTOTO WA JACKIE CHAN ASHITAKIWA KWA DAWA ZA KULEVYA
- MWENYEKITI WA PROIN, JOHNSON LUKAZA NA MDOGO WAKE ...
-
▼
December
(168)
0 comments:
Post a Comment