Friday, December 26, 2014

On 12:04 PM by Unknown   No comments
MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Mganda, Dan Sserunkuma ameanza kuonyesha cheche ndani ya kikosi hicho baada ya juzi Jumatano kufanikiwa kufunga mabao mawili na kuisaidia kuipa timu yake ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Taifa Jang’ombe katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.
Simba ambayo leo Ijumaa inatarajiwa kushuka kwenye Dimba la Taifa jijini Dar kuikabili Kagera Sugar katika Ligi Kuu Bara, ilionyesha kiwango kiwango kizuri katika mchezo huo uliochezwa usiku na kuhudhuriwa na mashabiki wengi.
Sserunkuma ambaye amesajiliwa na Simba katika dirisha dogo la usajili akitokea Gor Mahia ya Kenya alikuwa staa katika mchezo huo maalum kwa kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Kituo cha ITV/Radio One, Maulid Hamad.
Beki wa pembeni wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ndiye aliyeanza kufungua ukurasa wa mabao kwa kufunga katika dakika ya 73, Sserunkuma akaongeza la pili kwa penalti iliyotokana na Emmanuel Okwi kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari katika dakika 79 kisha kuongeza la tatu dakika ya 85.
Bao la kufutia machozi la wenyeji lilifungwa na Hafidhi Bariki katika dakika ya 69
Baada ya mechi hiyo Championi Ijumaa lilizungumza na Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri ambaye alisema kikosi chake kipo vizuri na zaidi anakazania kuwaunga wachezaji wapya na wa zamani ili kutengeneza kombinesheni nzuri.

0 comments:

Post a Comment