Saturday, December 20, 2014

On 2:06 PM by Unknown   No comments


Muonekano wa Jordan baada ya kujiongezea urembo kufanana na Kim.
Mwanaume aliyejitambulisha kwa jina la Jordan (23) amefanya mambo ya ajabu akijitahidi kufanana na Kim kwa kujiongeza urembo bandia, hasa kufanya midomo yake kuwa mikubwa akitaka ifanane na ya Kim.

Kim Kardashian katika pozi.
Ametumia Pauni 150,000 au dola laki mbili na arobaini katika harakati zake za kutaka kufanana kama Kim
Pesa hizo zote amezitumia kwa kufanyiwa upasuaji na kuongezwa urembo bandia.
Cha kushangaza ni kwamba huyu ni mwanamume anayetaka kufanana kama mwanamke
Aliambia jarida la The Sun kwamba alianza kumuenzi Kim Kardashian mwenye umri wa miaka 33 baada ya kutazama makala ya kipindi kijulikanacho kama ''Keeping Up With The Kardashians.'' Kipindi kinachohusu Kim na Familia yake. 'Ninapenda kila kitu kumhusu Kim,' aliambia The Sun. 'yeye ndiye mwanamke mrembo zaidi duniani. Ngozi yake ni nyororo, nywele zake zinapendeza yaani kila kitu kumhusu kinanipendeza. ''

Jordan ni kijana mwenye umri wa miaka 23 anashindana kufanana na Kim.
Jordan amefanyiwa upasuaji kuongeza urembo bandia zaidi ya mara 50 katika juhudi zake za kutaka kufanana kama Kim, amerembeshwa midomo, ametolewa nywele kwa kutumia miale ya Laser , amewekwa Tatoo na hata kubadilisha kope zake na mengine mengi.

Lakini mabadiliko haya yote yamemgeuza sura sana Jordan na kumanya kuwa kichekesho kwa watu wengi.

''Mimi mwenyewe hucheka watu wanapojaribu kunitusi au kunikejeli, na kuniambia kwamba mimi ni kama tu plastiki, yaani kila kitu mwilini mwangu ni baandia. Lakini hio hainijalishi.''

0 comments:

Post a Comment