Tuesday, December 16, 2014

On 4:42 AM by Unknown   No comments
Kilimanjaro Katika Kitongoji cha Njiapanda Magharibi (Vunjo) CCM ilishinda kwa kura (343), NCCR-Mageuzi (195) na TLP-(36). 
Katika Kitongoji cha Njiapanda Mashariki (Vunjo), NCCR-Mageuzi imeshinda kwa kura (277), CCM (239), Chadema (71) na TLP (37). Katika Kitongoji cha Faru (Vunjo) Chadema imeshinda kwa kura (288), CCM (93), TLP (27) na NCCR-Mageuzi (7). Katika Kitongoji cha Darajani (Vunjo), NCCR-Mageuzi imeshinda (208), CCM (204), Chadema(169) na TLP (46). Kitongoji cha Kashinda (Vunjo), NCCR-Mageuzi imeshinda kwa kura 31, CCM (19) na Chadema (13). Kitongoji cha Makere NCCR-Mageuzi imeshinda kwa kura 52, CCM (20). Kitongoji cha Ofisini Chadema imeshinda kwa kura 43, NCCR-Mageuzi (20) na CCM (12).

Katika Kijiji cha Marawe Kirua (Vunjo), CCM imeshinda kwa kura 164, Chadema (77), NCCR-Mageuzi (84) na TLP (43). Katika Manispaa ya Moshi Mtaa wa Rengua, Chadema imeshinda kwa kura 83 na CCM (58). Mtaa wa Bonitte, Chadema imeshinda kwa kura 65 na CCM (51). Mtaa wa Kiusa CCM imeshinda kwa kura 143 na Chadema (95). Mtaa wa Korongoni Chadema imeshinda kwa kura 252 na CCM (244). Mtaa wa Sabasaba CCM imeshinda kwa kura 228, Chadema (114) na katika Mtaa wa Kambaita CCM ilishinda kwa kura 172 na Chadema(171).
Arusha Chadema kimeendelea kukitesa CCM wilayani Karatu, baada ya kushinda viti 24 kati ya 27 katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Karatu. Katika Mtaa wa Mazingira Bora, Chadema ilishinda kwa kura 260, CCM kura 137. Kitongoji cha Bomani, Chadema ilishinda kwa kura 251 na CCM ilipata kura 177. Karatu Kati, Chadema kura 281, CCM, 109. Kigoma Katika Kata ya Mwandiga, Kigoma katika matokeo ya awali hadi tunakwenda mitamboni CCM ilikuwa imeshinda mitaa minane, ACT minane na ADC mtaa mmoja. Dar es Salaam Katika Mkoa wa Dar es Salaam, matokeo yalichelewa kutangazwa katika baadhi ya maeneo na kusababisha malalamiko kutoka kwa baadhi ya wapigakura waliokuwa wakihisi kuwapo kwa uchakachuaji. Katika Mtaa wa Kwa Mzungu, Kilungule, Temeke, CCM ilishinda kwa kura 378, CUF 303 na zilizoharibika ni 185. Katika Mtaa wa Kivukoni, CCM kimeshinda kwa kura 183, Chadema (65). Mtaa wa See View, CCM imepita bila kupingwa. Matokeo hayo yametangazwa na msimamizi msaidizi Renatus Luhungu. Mtaa wa Segerea Migombani, Chadema imeshinda kwa kura (547), CCM (273), NCCR-Mageuzi (205). Mtaa wa Hananasif Kinondoni, CCM imeshinda kwa kura 472, Chadema (231).

Kilindi

CCM imepita bila kupingwa katika vitongoji 615 na vijiji 102. Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Kilindi, Daudi Maige alisema jana kuwa kutokana na CCM kupita bila kupingwa katika vijiji 102 na vitongoji 615 uchaguzi ulilazimika kufanyika katika vijiji viwili tu, Kileguru na Makasini.


Mbeya

Mtaa wa Sabasaba nafasi ya Mwenyekiti CCM, Aidan Ng’oma, kura 74 wakati Anna Mwenda wa Chadema akipata kura 23. Mtaa wa Kisoki mgombea wa uenyekiti Edward Mwakasiti wa CCM alitangazwa mshindi baada ya kupita bila kupingwa.
Katika Mtaa wa Mwasyoke, uchaguzi wa mwenyekiti uliahirishwa, lakini kwa upande wa wajumbe, CCM ilipata viti vitatu wakati Chadema ilipata viwili. Mtaa wa Itezi, mgombea wa CCM, Anania Sanga alipita bila kupingwa, kama ilivyokuwa kwa Daud Kipenya wa chama hicho kwa Mtaa wa RRM.

Kutoka Vwawa mgombea wa uenyekiti Kitongoji cha Masaki (Chadema) alipata kura 96 wakati CCM ilipata kura 48.

0 comments:

Post a Comment