Saturday, January 3, 2015
On 2:53 AM by Unknown in Download No comments
WAZIRI wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais wa nchi anaswa akicheza sebene katika Kanisa la Efatha linaloongozwa na Nabii Josephat Mwingira, mjini Kibaha, Pwani.
Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiselebuka.
Nyalandu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM), alifanya hayo juzi katika mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2015 ambapo alipanda jukwaani na kusakata muziki huku akishangiliwa na waumini wa kanisa hilo.
Kuonesha msisitizo, Nabii Mwingira naye aliingilia jukwaani na kucheza muziki huo wa Injili huku akighani maneno ya Mungu kwa kutumia kipaza sauti alichokuwa nacho mkononi saa zote za hafla hiyo.
Mara baada ya saa sita na dakika 35 usiku kutimia Nyalandu ambaye alikuwa mgeni rasmi alikaribishwa kusema neno ambapo alipanda jukwaani na kumshukuru Mungu kwa kuuona mwaka mpya 2015.
Hata hivyo, alijipigia kampeni kwa kuwakumbusha waumini hao kuwa Oktoba mwaka huu Tanzania itakuwa na tukio kubwa, hivyo waumini hao kwake ni muhimu kwani wakati ukifika atawaomba kura zao.
“Wakati nacheza pale nimewaona wanakwaya na kuhisi kwamba wana kitu moyoni. Nawaambia Oktoba ikifika lazima mchague vijana nami nitawahitaji sana kuja kuniimbia,” alisema.
“Wakati nacheza pale nimewaona wanakwaya na kuhisi kwamba wana kitu moyoni. Nawaambia Oktoba ikifika lazima mchague vijana nami nitawahitaji sana kuja kuniimbia,” alisema.
Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwa na viongozi wa kanisa.
Naye Nabii Mwingira alisema mwaka 2015 anatamka wale wote ambao wapo kanisani hapo na wana dhamira moyoni mwao, watatimiziwa na Mungu wa Efatha.
“Huwa sisi hatuamini katika mashetani, tunaamini katika roho saba... hivyo natamka kwamba wote waliopo hapa na wana nia zao katika vifua vyao, basi Mungu atawapa,” alisema Mwingira huku akishangiliwa.
Hii ni mara ya pili kwa Nyalandu kujipigia kampeni za urais kanisani, mara ya kwanza ni hivi karibuni katika jimbo lake alipokwenda katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kijijini Ilongelo, Singida.
Kiongozi huyo pia alikwenda katika Shule ya Msikiti wa Ilongelo ambapo inadaiwa alitoa msaada wa kusaidia shule na kanisa hilo.
Kiongozi huyo pia alikwenda katika Shule ya Msikiti wa Ilongelo ambapo inadaiwa alitoa msaada wa kusaidia shule na kanisa hilo.
Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Hata hivyo, baadhi ya wadau wa siasa waliozungumza na gazeti hili juzi jijini Dar walisema kuwa anachofanya Nyalandu ni kinyume na maadili ya chama chake ambacho kinakataza kutumia makanisa na misikiti kujipigia debe katika mambo ya siasa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Taifa wa CCM, Nape Nnauye hakupatikana ili aweze kutoa maoni yake kuhusu vitendo hivyo kwani simu yake ilikuwa haipatikani.
Baadhi ya wagombea waliotangaza nia kutoka CCM ni Dk Hamisi Kigwangalla, Januari Makamba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na wengine wanaotajwatajwa ni Steven Wassira, Bernard Membe, Samwel Sitta na Edward Lowassa.
Baadhi ya wagombea waliotangaza nia kutoka CCM ni Dk Hamisi Kigwangalla, Januari Makamba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na wengine wanaotajwatajwa ni Steven Wassira, Bernard Membe, Samwel Sitta na Edward Lowassa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Search
Translate
Popular Posts
-
Leo wanawake wenzangu kwenye safu yetu hii pendwa nimewaletea mada moja nzito ambayo ukiiendekeza unavunja nyumba yako hivihivi unajiona.H...
-
Utandawazi utawaabisha wengi kwani hizi simu zetu ukizubaa kidogo mtu anakupiga picha hata kama hujadhamiria kufanya hivi.
-
Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela AIBU ilioje! Denti wa chuo kimoja jijini Dar, anayefahamika kwa jina moja la Martha, amepiga...
-
Hebu niambie...umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi, umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? ...
-
Wanachuo wazidi kuwa mfano mbaya licha kuonekana wasomi na ndio tegemeo kwa taifa la kesho lakini cha ajabu wanazidi kufanya madudu badal...
-
MDADA MWENYEWE NI HUYU. DENT mmoja katika Chuo Kikuu kimojawapo hapa nchini amepiga picha zisizo na maadili akiwa na njemba wake katika ...
-
Kweli dunia inamambo watu kadhaa wamekamatwa na kamera zetu wkingonoka bila uoga wowote tena hadharani hebu ona picha hapa
-
Hivi Majuzi mke wa Mchungaji mmoja amekamatwa laivu akingonoka vichakani umbali kidogo kutoka katika nyumbani kwake Mke wa Mchungaji a...
-
Polisi mkoani Tanga wamesema wataendesha msako wa kuwakamata watu wanaofanya biashara ya ngono katika nyumba za starehe na mitaa maarufu ...
Blog Archive
-
▼
2015
(18)
-
▼
January
(18)
- NDOA YA LULU YABUMA!
- DIAMOND PLATNUMZ AFUNIKA SIKU YA MWAKA MPYA KIGALI...
- MAJENGO YABOMOKA MENGINE HATARINI KUWAANGUKIA WATO...
- URAIS 2015: NYALANDU AKESHA AKICHEZA SEBENE!
- WEMA:Van Vicker Alichangia Niachane na Diamond
- "Sijawahi kutoa wala kupokea Rushwa na bado nina d...
- Mke wa Mtu Asaula Nguo Akimfuta Jasho Bi. Harusi
- Jokate Ampa Makavu Diamond.......Asema hana Akili ...
- Aunt Ezekiel: Mume wangu Hajui kama nina Mimba
- Jokate: Sipendi Kutomaswa Kwenye Filamu za Mambo y...
- DAH NENO MOJA KWA HUYU MWANADADA>>>HIVI ATAKUWA AN...
- HUYU NDIO MWANA MAMA MWENYE MAZIWA MAKUBWA ZAIDI H...
- Elimu ya Sekondari itakuwa BURE kuanzia 2016 - Jak...
- Werema apokelewa kwa furaha kijijini kwake
- TAMBUA VIMBE MBALIMBALI KWA MWANAMKE NA JINSI YA K...
- AIBU FUNGA MWAKA! MREMBO WA BONGO MOVIE ANASWA USI...
- USIWE MBULULA, UNA HAKI YA KUPENDA ILA ‘USIFOSI’ M...
- ROSE MHANDO ATUMBUIZA NA KITUMBO
-
▼
January
(18)
0 comments:
Post a Comment