Saturday, January 3, 2015

On 3:05 AM by Unknown in    No comments

Mwigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

BAADA ya kuwa na malengo ya kuolewa mwaka 2014, mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibuka na kusema imeshindikana lakini hajilaumu wala hamlaumu mtu yeyote kwa kutotimiza suala hilo kwani anaamini Mungu ndiye anayewezesha kila kitu.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Lulu alisema mwaka 2014 alikuwa na malengo mengi likiwemo suala la ndoa lakini kwa kuwa Mungu ndiye muweza, atapanga upya suala hilo na anaamini litakuja kutimia.

“Ndoa ni mipango ya Mungu, huwezi kulazimisha hata siku moja, sisi wanadamu huwa tuna mipango yetu lakini ili ifanikiwe lazima kuwe na baraka za Mungu,” alisema Lulu.
Akizidi kupiga stori na paparazi wetu, Lulu alisema kwa mwaka huu na mwakani hawezi kuweka malengo ya ndoa kwani bado kuna mambo yake hajayaweka sawa hivyo suala la kuolewa ataliweka hadharani baada ya miaka miwili ijayo.

Lulu’ akipozi.
“Sina mpango hata kidogo kwa mwaka huu wala mwakani labda baada ya hii miaka kupita ndiyo ninaweza kupanga tena suala la ndoa,” alisema Lulu.
Alipotakiwa kumtaja mpenzi aliyenaye kwa sasa, Lulu aligoma kufunguka lakini akakubali kuanika siri za mwanaume anayetaka kuwa mumewe.
“Kwanza nahitaji mwanaume atakayenielewa kwa kila kitu, pia awe na mapenzi ya kweli na atakayeniangalia kama Lulu na siyo kama Elizabeth pekee. Anapaswa kutambua na kusapoti kazi zangu za sanaa,” alisema Lulu.
Kuhusu mikakati yake ya sanaa mwaka huu, Lulu alisema ana mpango wa kuendelea na masomo huku akiwa pia na ‘project’ kubwa mbili ambazo anatarajia kuzifanya.
“Nina project kubwa mbili mwaka huu, muda utakapofika kila mmoja atazijua maana 
On 3:01 AM by Unknown in    No comments


Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa amebebwa na wacheza shoo wake siku ya mwaka mpya Kigali, Rwanda.



Diamond Platnumz akifanya yake.



Nyomi ya kufa mtu waliofika siku ya shoo hiyo.



Akifanya yake na wacheza shoo wake.



Mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' mpenzi mpya wa Diamond Platnumz akiwa katika pozi.



Muonekano wa siku ya shoo hiyo.



Diamond Platnumz (katikati) akifanya yake akiwa na Yamoto Bendi.
On 2:56 AM by Unknown in    No comments


Diwani wa kata ya Kibindu Mawazo Mkufya aliyenyanyua mikono juu akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kulia aliyevaa kofia ya kijani kufuatia mvua kubwa kubomoa madarasa ya shule ya Msingi Kibindu.



Moja ya darasa la shule ya msingi Kibindu likiwa limebomoka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa mwaka jana.



Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa Habari mbele ya jengo la shule ya Msingi Kibindu ambalo lilianguka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa mwaka jana kushoto ni diwani wa kata ya Kibindu Mawazo Mkufya.



Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa Kata ya Kibindu alipofika kuwajulia hali kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa mwaka jana.
WANAFUNZI wa shule ya Msingi Kibindu wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wako hatarini kuangukiwa na vyumba vya madarasa wanayosomea kutokana na ubovu wa vyumba hivyo ambavyo vimejengwa miaka ya 50.
Mwishoni mwa mwaka jana vyumba vya madarasa mawili na ofisi ya mwalimu vilianguka na kuezua mapaa ya vyumba vine vya madarasa na ofisi ya mwalimu mkuu baada ya kutokea mvua kubwa amabyo iliambatana na kimbunga.
Shule hiyo ambayo ina wanafunzi 970 hawakuwepo shuleni kwani walikuwa wako likizo ya mwisho wa mwaka baada ya shule kufungwa mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete ambaye alitembelea shuel hiyo ofisa mtendaji wa kijiji cha kibindu Juma Athuman alisema kuwa mvua hiyo kubwa iliambatana na kimbunga ilinyesha Desemba 28 mwaka jana  na kuangusha majengo mawili ya madarasa pamojana na kueezua mapaa ya vyumba  vinne vya madasa na  na ofisi ya mwalimu mkuu.
Athuman alisema kuwa kimunga hicho pia kilisababisha ufa katika majengo mengine kadhaa ya madarasa katika shule hiyo na  kuwa katika hatari kubwa ya kuanguka.“Hali hiyo inatia wasiwasi kwa wanafunzi wnaotarajiwa  kuanza  masomo Januari  14 mwezi huu kuwa hatarini kuangukiwa na majengo hayo endapo hatua za dharura hazitachukuliwa,” alisema Athuman.

Akizungumzia  mara  baada ya kutembelea shule hiyo  Mbunge wa Jimbo la Chalizne Ridhiwani Kikwete amesikitishwa na hali hiyo ya majengo ya shule hiyo  na kusema kuwa anafanya taratibu za kuwasiliana na mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kuona jinsi ya kujenga upya shule hiyo.
On 2:53 AM by Unknown in    No comments


WAZIRI wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais wa nchi anaswa akicheza sebene katika Kanisa la Efatha linaloongozwa na Nabii Josephat Mwingira, mjini Kibaha, Pwani.



Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiselebuka.
Nyalandu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM), alifanya hayo juzi katika mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2015 ambapo alipanda jukwaani na kusakata muziki huku akishangiliwa na waumini wa kanisa hilo.
Kuonesha msisitizo, Nabii Mwingira naye aliingilia jukwaani na kucheza muziki huo wa Injili huku akighani maneno ya Mungu kwa kutumia kipaza sauti alichokuwa nacho mkononi saa zote za hafla hiyo.
Mara baada ya saa sita na dakika 35 usiku kutimia Nyalandu ambaye alikuwa mgeni rasmi alikaribishwa kusema neno ambapo alipanda jukwaani na kumshukuru Mungu kwa kuuona mwaka mpya 2015.
Hata hivyo, alijipigia kampeni kwa kuwakumbusha waumini hao kuwa Oktoba mwaka huu Tanzania itakuwa na tukio kubwa, hivyo waumini hao kwake ni muhimu kwani wakati ukifika atawaomba kura zao.
“Wakati nacheza pale nimewaona wanakwaya na kuhisi kwamba wana kitu moyoni. Nawaambia Oktoba ikifika lazima mchague vijana nami nitawahitaji sana kuja kuniimbia,” alisema.

Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwa na viongozi wa kanisa.
Naye Nabii Mwingira alisema mwaka 2015 anatamka wale wote ambao wapo kanisani hapo na wana dhamira moyoni mwao, watatimiziwa na Mungu wa Efatha.
“Huwa sisi hatuamini katika mashetani, tunaamini katika roho saba... hivyo natamka kwamba wote waliopo hapa na wana nia zao katika vifua vyao, basi Mungu atawapa,” alisema Mwingira huku akishangiliwa.
Hii ni mara ya pili kwa Nyalandu kujipigia kampeni za urais kanisani, mara ya kwanza ni hivi karibuni katika jimbo lake alipokwenda katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kijijini Ilongelo, Singida.
Kiongozi huyo pia alikwenda katika Shule ya Msikiti wa Ilongelo ambapo inadaiwa alitoa msaada wa kusaidia shule na kanisa hilo.
Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Hata hivyo, baadhi ya wadau wa siasa waliozungumza na gazeti hili juzi jijini Dar walisema kuwa anachofanya Nyalandu ni kinyume na maadili ya chama chake ambacho kinakataza kutumia makanisa na misikiti kujipigia debe katika mambo ya siasa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Taifa wa CCM,  Nape Nnauye hakupatikana ili aweze kutoa maoni yake kuhusu vitendo hivyo kwani simu yake ilikuwa haipatikani.
Baadhi ya wagombea waliotangaza nia kutoka CCM ni Dk Hamisi Kigwangalla, Januari Makamba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na wengine wanaotajwatajwa ni Steven Wassira, Bernard Membe, Samwel Sitta na Edward Lowassa.